Matthew 24:32-35

32 a“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 33 bVivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 34 cAmin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 35 dMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

(Marko 13:32-37; Luka 17:26-30, 34-36)

Copyright information for SwhKC